Moha Jicho Pevu: Niko tayari kufa, sitishiki:
Shikamoo Meja mstaafu Joseph Nkaissery. Natumai u buheri wa afya
popote ulipo chini ya ulinzi mkali unaotokana na ushuru wangu na Wakenya
wenzangu.
Wiki iliyopita, nilipokuwa nikitazama sherehe za Jamuhuri ya
Kenya, twasira yako ilinijia na kutaka kujua ni kwa nini tuwe katika
hali ya utumwa tukisheherekea miaka 52 ya uhuru wa taifa hili. Wiki hio
hiyo, nikiwa futi kadhaa angani kutoka Mandera, niliarifiwa kuwa
ulinitaja jina, sio mara moja, bali mara kadhaa na kuonekana kujaribu
kuhusisha jina langu na wanamgambo wa Al-Shabaab, eti nilikuwa
nikipasisha ujumbe wao na kutokuwa mzalendo mpenda taifa.
Naarifiwa pia ulitutaka, sijui kama ni mimi na Yassin Juma, tuombe
msamaha kwa kutoa taarifa za kutatanisha. Naomba kwa heshima nikuweke
sawa mzee wangu.
Kwanza kabisa, siombi msamaha maana sijui kosa langu ni lipi.
Pili, wa kuomba msamaha ni wewe kwa kutuhusisha sisi wawili na ugaidi
ukitumia wadhifa wako, huku ukilegeza kamba kwa kuchagua wanahabari
wawili kati ya wote walioripoti tukio hilo. Je, ulituchagua kwa sababau
sisi ni Waisilamu Je, ulituchagua kwa sababu sisi hatukubaliani na kauli
ya serikali Je, ulituchagua kutokana na msukumo wa wale maskauti wa
propaganda 36 wa serikali Nauliza unijibu.
Taarifa hizo zilisemwa na wengi, lakini ikija kwangu sijui ni
dini, kazi yangu murwa, jina langu au msimamo wangu. Ningelipenda
kukukumbusha kuwa kuna msemo unaosema mti mwenye matunda ndio upigwao
mawe.
Naona serikali imenichagua kuwa mti huo kwa sasa. Sitaomba
msamaha kwa kusema baadhi ya viongozi serikalini ni wafisadi; sitaomba
msamaha kwa kusema tangu uhuru wa taifa hili, kuna mauaji ya kiholela
Kenya; sitaomba msamaha kwa kusema bunge letu limejaa mafisadi; sitaomba
msamaha kwa kusema serikali iliyo mamlakani imetufeli kwa kutotimiza
ahadi zetu, ahadi ilizotuahidi wakati wa kampeni zake; sitaomba msamaha
kwa kuuliza ni nani aliyejaribu kupora ardhi ya shule ya msingi ya
Lang’ata; sitaomba msamaha kwa kuuliza ni nani anayeua vijana humu
nchini kama inavyoripotiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu humu
nchini na hata nje; sitaomba msamaha kwa kuuliza pesa za NYS zililiwa
na nani; sitaomba msamaha kwa kuuliza senti za Eurobond; sitaomba
msamaha kwa kuuliza senti za Anglo-Leasing; sitaomba msamaha kwa
kuwakemea baadhi ya viongozi kukoma kuwatenganisha Wakenya kwa misingi
ya kikabila na matamshi yao ya chuki, juu ya haya yote, sitaomba msamaha
mtu binafsi bali nitamwomba aliye juu Mbinguni anayestahili sifa.
Kama nikuomba msamaha bwana Nkaisserry basi naomba msamaha wa
kuzungumza ukweli na kuzidi kuzungumza ukweli kila kukicha. Kumbuka
tumeona wengi wakija na kuondoka. Tumeona wengine wakiapa hawatajiuzulu
labda wafe. Hata maisha yangu yakitishiwa, nitasimama kidete. Ni kwa
nini unachafua jina na hunijui, wala hatujawahi zungumza. Je, ulinialika
afisini mwako Je, ulitaka kujua kiini cha habari hizo zilitoka wapi La,
hasha!
Inakuaje walio mamlakani wana haki ya kuniita gaidi, kunitusi na
hata kunitishia Kumbuka kuwa Mungu halali ni mkuu na atatulipia. Naomba
uniskize Bwana Waziri, japo mdogo wako ki umri na fikra. Kwa mtazamo wa
wengi na hata wadadisi wa masuala ya kisiasa, gaidi mkubwa zaidi duniani
ni serikali isiyojali watu wake na kuwahudumia ipasavyo.
Gaidi ni serikali inayowaibia watoto wake. Gaidi ni serikali
iliyojawa na ufisadi. Gaidi ni serikali inayogawanya wananchi wake kwa
misingi ya kikabila. Gaidi ni serikali inayokuza chuki na uhasama
miongoni mwa watu wake. Gaidi ni serikali isoyodhamini uhai wa binadamu.
Gaidi ni serikali isiyotatua matatizo ya kila siku ya wananchi wake.
Kama alivyonena Robert A Heinlein, “When any government, or any
church for that matter, undertakes to say to its subject, ‘This you may
not read, this you must not see, this you are forbidden to know,’ the
end result is tyranny and oppression no matter how holy the motives”
Naarifiwa vita hivi vyote dhidi yangu ni kwa sababu za kisiasa.
Mwanipeleka mbio kama gari mpya mkihofia nitainingi siasa Mimi ni
mwanahabari kwa sasa. Mbona mwaeneza chuki na fitina dhidi yangu Leo
nawakumbusha kuwa msafara wa mamba ndani yake kuna mburukenge, kwa hivyo
mshistuke! Ketini mkijua pindi mwakani salamu zitawajia na mkumbuke si
kila anayeishi mahakamani anajua sheria. Kwa sababu ya vitisho hivyi,
nikifa leo au kesho, wakulaumiwa atajulikana. Lakini mimi siogopi kufa.
Msijaribu kuturudisha katika enzi za Kanu. Hilo haliwezekani maana ni
sawia na kutia gunia upepo.
Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN.
Kuwasiliana naye: thenairobian@standardmedia.co.ke;
mali@standardmedia.co.ke; FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali;
Twitter: @mohajichopevu
Moha Jicho Pevu: Niko tayari kufa, sitishiki:
Shikamoo Meja mstaafu Joseph Nkaissery. Natumai u buheri wa afya popote ulipo chini ya ulinzi mkali unaotokana na ushuru wangu na Wakenya wenzangu.
Wiki iliyopita, nilipokuwa nikitazama sherehe za Jamuhuri ya Kenya, twasira yako ilinijia na kutaka kujua ni kwa nini tuwe katika hali ya utumwa tukisheherekea miaka 52 ya uhuru wa taifa hili. Wiki hio hiyo, nikiwa futi kadhaa angani kutoka Mandera, niliarifiwa kuwa ulinitaja jina, sio mara moja, bali mara kadhaa na kuonekana kujaribu kuhusisha jina langu na wanamgambo wa Al-Shabaab, eti nilikuwa nikipasisha ujumbe wao na kutokuwa mzalendo mpenda taifa.
Naarifiwa pia ulitutaka, sijui kama ni mimi na Yassin Juma, tuombe
msamaha kwa kutoa taarifa za kutatanisha. Naomba kwa heshima nikuweke
sawa mzee wangu.
Kwanza kabisa, siombi msamaha maana sijui kosa langu ni lipi.
Pili, wa kuomba msamaha ni wewe kwa kutuhusisha sisi wawili na ugaidi
ukitumia wadhifa wako, huku ukilegeza kamba kwa kuchagua wanahabari
wawili kati ya wote walioripoti tukio hilo. Je, ulituchagua kwa sababau
sisi ni Waisilamu Je, ulituchagua kwa sababu sisi hatukubaliani na kauli
ya serikali Je, ulituchagua kutokana na msukumo wa wale maskauti wa
propaganda 36 wa serikali Nauliza unijibu.
Taarifa hizo zilisemwa na wengi, lakini ikija kwangu sijui ni dini, kazi yangu murwa, jina langu au msimamo wangu. Ningelipenda kukukumbusha kuwa kuna msemo unaosema mti mwenye matunda ndio upigwao mawe.
Naona serikali imenichagua kuwa mti huo kwa sasa. Sitaomba msamaha kwa kusema baadhi ya viongozi serikalini ni wafisadi; sitaomba msamaha kwa kusema tangu uhuru wa taifa hili, kuna mauaji ya kiholela Kenya; sitaomba msamaha kwa kusema bunge letu limejaa mafisadi; sitaomba msamaha kwa kusema serikali iliyo mamlakani imetufeli kwa kutotimiza ahadi zetu, ahadi ilizotuahidi wakati wa kampeni zake; sitaomba msamaha kwa kuuliza ni nani aliyejaribu kupora ardhi ya shule ya msingi ya Lang’ata; sitaomba msamaha kwa kuuliza ni nani anayeua vijana humu nchini kama inavyoripotiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu humu nchini na hata nje; sitaomba msamaha kwa kuuliza pesa za NYS zililiwa na nani; sitaomba msamaha kwa kuuliza senti za Eurobond; sitaomba msamaha kwa kuuliza senti za Anglo-Leasing; sitaomba msamaha kwa kuwakemea baadhi ya viongozi kukoma kuwatenganisha Wakenya kwa misingi ya kikabila na matamshi yao ya chuki, juu ya haya yote, sitaomba msamaha mtu binafsi bali nitamwomba aliye juu Mbinguni anayestahili sifa.
Kama nikuomba msamaha bwana Nkaisserry basi naomba msamaha wa kuzungumza ukweli na kuzidi kuzungumza ukweli kila kukicha. Kumbuka tumeona wengi wakija na kuondoka. Tumeona wengine wakiapa hawatajiuzulu labda wafe. Hata maisha yangu yakitishiwa, nitasimama kidete. Ni kwa nini unachafua jina na hunijui, wala hatujawahi zungumza. Je, ulinialika afisini mwako Je, ulitaka kujua kiini cha habari hizo zilitoka wapi La, hasha!
Inakuaje walio mamlakani wana haki ya kuniita gaidi, kunitusi na hata kunitishia Kumbuka kuwa Mungu halali ni mkuu na atatulipia. Naomba uniskize Bwana Waziri, japo mdogo wako ki umri na fikra. Kwa mtazamo wa wengi na hata wadadisi wa masuala ya kisiasa, gaidi mkubwa zaidi duniani ni serikali isiyojali watu wake na kuwahudumia ipasavyo.
Gaidi ni serikali inayowaibia watoto wake. Gaidi ni serikali iliyojawa na ufisadi. Gaidi ni serikali inayogawanya wananchi wake kwa misingi ya kikabila. Gaidi ni serikali inayokuza chuki na uhasama miongoni mwa watu wake. Gaidi ni serikali isoyodhamini uhai wa binadamu. Gaidi ni serikali isiyotatua matatizo ya kila siku ya wananchi wake.
Kama alivyonena Robert A Heinlein, “When any government, or any church for that matter, undertakes to say to its subject, ‘This you may not read, this you must not see, this you are forbidden to know,’ the end result is tyranny and oppression no matter how holy the motives”
Naarifiwa vita hivi vyote dhidi yangu ni kwa sababu za kisiasa. Mwanipeleka mbio kama gari mpya mkihofia nitainingi siasa Mimi ni mwanahabari kwa sasa. Mbona mwaeneza chuki na fitina dhidi yangu Leo nawakumbusha kuwa msafara wa mamba ndani yake kuna mburukenge, kwa hivyo mshistuke! Ketini mkijua pindi mwakani salamu zitawajia na mkumbuke si kila anayeishi mahakamani anajua sheria. Kwa sababu ya vitisho hivyi, nikifa leo au kesho, wakulaumiwa atajulikana. Lakini mimi siogopi kufa. Msijaribu kuturudisha katika enzi za Kanu. Hilo haliwezekani maana ni sawia na kutia gunia upepo.
Mohammed Ali ni Mhariri Mkuu wa Kitengo cha Upekuzi KTN. Kuwasiliana naye: thenairobian@standardmedia.co.ke; mali@standardmedia.co.ke; FB: Official Jicho Pevu with Mohammed Ali; Twitter: @mohajichopevu
He remembers the exact
time he noticed his son Jonathan Wasike was missing. He even remembers
what he was doing when it dawned on him that he couldn't see his first
born child.
Jeremiah Ndombi and his 4-year-old son Jonathan Wasike. (PHOTO: MOSES
OMUSULA/ STANDARD)
"It was 3.13 pm and I was heading towards the parking lot when I
realised Jonathan was not in the vicinity," said Mr Ndombi.
While they had remained at the lunch table, Jonathan had joined other
children at the club's playground just a few metres from where they were
seated.
Ndombi suspects that Jonathan might have left the playground to follow
his father, but when his father disappeared among other people,
oblivious of his son behind him, he left the club.
It is then that the search begun in earnest, with the family members
making frantic calls to their relatives to come and help them comb
through the club to find Jonathan.
See also: Day my prodigal son returned
"I was at home when I got the news. I rushed to Impala and we searched
everywhere. We even went to the pool and contemplated draining the water
in case he had drowned," said Jonathan's uncle Lawrence Ndombi.
By 5.30 pm, they hadn't found him. They broadened their search to social
networks where they splashed his photo with an appeal that anyone who
would have seen him to report to the police.
Before long, the photo was being shared and circulated by several
people. The Standard Digital is among the platforms that the family used
to ensure the message of Jonathan's disappearance reached many people.
Their journey back home began way past 2.00 am when they had searched
all possible places the child would have been.
Checking Impala Club's CCTV cameras took a while, but by the time they
accessed footage of the day's event, they saw Jonathan walking out of
the club.
"The security guards at the gate had told us they didn't see a child
walking out, but the cameras showed him disappearing outside the
compound," said Jonathan'
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Joy as Jeremiah Ndombi's boy lost at Impala club reunites with parents
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Joy as Jeremiah Ndombi's boy lost at Impala club reunites with parents
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Joy as Jeremiah Ndombi's boy lost at Impala club reunites with parents
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Joy as Jeremiah Ndombi's boy lost at Impala club reunites with parents
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
Read more at: http://www.standardmedia.co.ke/article/2000185994/joy-as-boy-lost-at-impala-club-reunites-with-parents/
No comments:
Post a Comment